- Mteja anatakiwa awe na SIM iliyo halali na iliyosajiliwa ipasavyo iliyotolewa kwa mujibu wa kanuni za kumjua mteja pamoja na sheria na kanuni nyengine kuhusiana na usajili wa simu katika Jamhuri ya Muungano wa Tanania kama zitakavyorekebishwa mara kwa mara.
- Kutoa taarifa kwa Zantel haraka iwezekanavyo panapotokea wizi au upotevu wa SIM card.
- Kutoa taarifa kwa haraka Zantel pale panapokuwa na wasiwasi au tuhuma za vitendo vya utakasaji wa fedha haramu.
- Kuiarifu haraka Zantel baada ya kugundua wizi, ulaghai, upotevu, matumizi yasiyoruhusiwa au tukio jengine lolote haramu kuhusu akaunti/masuala ya EzyPesa.
- Tunza nywila yako kwa usalama na usiri wa akaunti yako ya Ezypesa