- Kujiunga piga *149*15# ,au atajiung kupitia menu ya Ezepesa *150*02# au afike kwa wakala wa mimina
- Kuna aina 3 za bando la intaneti – bando la siku, bando la wiki na bando la mwezi
- Bando ya siku inaweza kutumika kwa saa 24 tu
- Bando ya wiki inatumika kwa saa 168 tu
- Bando ya mwezi itatumika kwa saa 720
- Pia Mteja atapata ujumbe wa kiwango cha matumizi yake ya bando husika yakifikia 50%,80% na 100%.
- Kama mteja atajiunga na kifurushi hicho hicho kabla ya muda wa hicho kifurushi kuisha MB/GB zilizobakia zitajumlishwa kwenye MB/GB za kifurushi kipya na muda wa kutumika utakuawa wa hiki kifurushi kipya.
- Matumizi ya data alizonunua mteja zitatumika kulingana na mahitaji ya mteja mwenyewe kwa hivyo mteja anaweza kumaliza bando yote kabla ya kipindi cha bando kuisha, hivyo basi mteja anaweza kuruhusu ikiwa kifurushi chake kitaisha basi salio kuu litumike au kama salio la kifurushi litaisha basi huduma isimamishe,
- Mteja anaweza kufanya hivyo kwa kupiga *149*15# kisha achague namba 7 huduma kwa wateja na kisha namba ana afuatishe maelezo ya kuchagua kile atakacho.
- Ikitokea mteja hajafanya chaguo lolote kama ilivyoanishwa hapo kwenye pointi na 8 hapo juu na akawa amemaliza kifurushi chake Zantel in haki ya kuendelea kumpa huduma kama atakuwa na salio kutoka kwenye salio kuu.
- Bei zote zina Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT inclusive)
Matumizi ya bando ni matumizi ya mteja mwenyewe kwa hivyo mteja anaweza kumaliza bando yote kabla ya kipindi cha bando kuisha, ikitokea hivyo, muda wa hewani wa akaunti nyingine au akaunti kuu utatumika. Walakini katika tukio ambalo mteja akinunua bando jingine lenye bei na muda wa kutumika sawa na alilonunua kabla na pia kabla lile la awali halijamalizika, uhalali na muda wa bando jipya ndio utakaotumika.