loader
 • English English
 • Swahili Kiswahili
 • Mipito ya SDH na IP

  img

  Mfumo wa kable za EASSy ni mfumo wenye urefu wa kilomita 11,000 iliyo jengwa kwenye pwani ya Afrika Mashariki. Asilimia 92 inamilikiwa na Waafrika na asilimia 8 ni kampuni za simu za nje. Ina vituo kwenye nchi 9 na imeungana na angalau nchi 10 zisizo na pwani ambazo sasa hazitahitaji kutegemea satelaiti ili kupata huduma ya intaneti.

  • Inaunga zaidi ya vituo 500 kwenye nchi 30 za Kiafrika na sasa hivi inafika miji mia kwenye nchi 29 za Ulaya. Pia inafika kwenye miji 700 kwenye nchi 70 duniani. Inafika kutokea Mtunzini nchini Afrika Kusini mpaka bandari ya Sudan nchini Sudan.
  • Inaungana na kable nyingi za manowari mpaka Ulaya, Marekani, Uarabuni na Asia.
  • Ina mkonga peya mbili zinazo ungana na nchi 21 za Kiafrika na pia vituo 9 tofauti vya kimataifa.

  KITUO CHA UTUNZAJI EASSY CABLE (DAR ES SALAAM)

  Mfumo wa kable za Europe India Gateway (EIG) ni mfumo wa mawasiliano ya manowari inayo unganisha Uingereza, Portugal, Gibraltar, Monaco, Ufaransa, Libya, Misri, Saudi Arabia, Djibouti, Oman, UAE na India. EIG ni mfumo wa kwanza wa kiwango kikubwa cha mkonga wa mawasiliano kutoka Uingereza mpaka India.

  Zantel Park ni moja kati ya vituo 9 vya mfumo wa kable za EASSy . Kituo hichi kiko Zantel Park, Kiwanja namba 123, Mwai Kibaki Road, Msasani jijini Dar es Salaam, nchini Tanzania. Inasimamiwa na Zantel inayo unga kable za EASSy na SEAS. Kituo hichi kinahudumia nchi za jirani zisizo na pwani kama Rwanda, Burundi, Malawi na Zambia.

  Zantel pia inasimamia mfumo wa cable za Seychelles East Africa Submarine (SEAS) iliyo na kituo Zantel Park na kuungana na EASSy.

  MFUMO WA NYAYA UNAOTOKA ULAYA MPAKA INDIA

  • Ina urefu wa kilomita 15,000.
  • Inauwezo wa kufikisha terabits 3.84 kwa sekunde moja
  • Mfumo wa kable imeundwa na Alcatel-Lucent na TE Subcom (iliyo kuwa inafahamika kama Tyco)