loader
 • English English
 • Swahili Kiswahili
 • anza kutumia ezypesa

  img

  Kutumia huduma za Ezypesa unahitaji kujisajili kwa wakala wowote wa Ezypesa au duka la Zantel. Unahitaji

  • SIM kadi ya Zantel
  • Simu ya kiganjani

  Temblea wakala wowote wa EzyPesa alie karibu yako ama duka la Zantel na nyaraka zifuatazo:

  • Kitambulisho cha taifa; au
  • Kitambulisho cha kupigia kura; au
  • Kitambulisho cha kazini; au
  • Kitambulisho cha usalama wa jamii; au
  • Barua kutoka kwa serikali za mtaa.

  Vigezo na Masharti vya EzyPesa

  Utatakiwa kujaza fomu ya usajili wa wateja, kumbuka kusoma vigezo na masharti. Baada ya usajili piga *150*02# na chagua huduma unayohitaji. Mteja anatakiwa kubadilisha namba yake ya siri pale ambapo ataanza kutumia huduma ya Ezypesa.

  Majukumu ya Mteja wa Ezypesa

  • Mteja anatakiwa awe na SIM iliyo halali na iliyosajiliwa ipasavyo iliyotolewa kwa mujibu wa kanuni za kumjua mteja pamoja na sheria na kanuni nyengine kuhusiana na usajili wa simu katika Jamhuri ya Muungano wa Tanania kama zitakavyorekebishwa mara kwa mara.
  • Kutoa taarifa kwa Zantel haraka iwezekanavyo panapotokea wizi au upotevu wa SIM card.
  • Kutoa taarifa kwa haraka Zantel pale panapokuwa na wasiwasi au tuhuma za vitendo vya utakasaji wa fedha haramu.
  • Kuiarifu haraka Zantel baada ya kugundua wizi, ulaghai, upotevu, matumizi yasiyoruhusiwa au tukio jengine lolote haramu kuhusu akaunti/masuala ya EzyPesa.
  • Tunza nywila yako kwa usalama na usiri wa akaunti yako ya Ezypesa

  Majukumu ya zantel

  • Zantel kwa haraka itaifunga SIM Card iliyopotea, iliyoibiwa au iliyoharibika ili kuzuia mawasiliano mara tu baada kupokea taarifa kutoka kwa mteja.
  • Bila ya taarifa au kuridhia kwa mteja, Zantel kwa haraka itaifunga akaunti yoyote ya Ezypesa pale mteja/mtumiaji atakapoingiza neno siri au taarifa nyengine zisizo sahihi kwa zaidi ya mara tatu wakati akitumia huduma ya EzyPesa.
  • Akaunti yoyote ya EzyPesa iliyofungwa inaweza kufunguliwa baada ya masaa 48.
  • Zantel haitokuwa dhamana wala hasara yoyote itakayopatikana kutokana na kushirikiana kusiko halali katika matumizi ya neno siri.
  • Zantel inawajibika kufikisha taarifa kuhususiana na miamala yenye mashaka ya utakasishaji wa fedha haramu katika mamlaka husika.